Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 5:14-23 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Kuzimu inawangoja kwa hamu kubwa,imepanua kinywa chake mpaka mwisho.Waheshimiwa pamoja na raia wa Yerusalemuwanaingia humo makundi kwa makundi,kadhalika na wote wanaousherehekea.

15. Kila mtu atafedheheshwa,na wenye kiburi wote wataaibishwa.

16. Lakini Mwenyezi-Mungu wa majeshi atatukuzwa.Yeye huonesha ukuu wakekwa matendo yake ya haki,kwa kuwahukumu watu wake.

17. Wanakondoo, wanambuzi na ndama,watapata malisho yao kwenye magofu ya miji yao,kana kwamba hizo ni sehemu za malisho yao.

18. Ole wao wanaoburuta uovu kama kwa kamba;wanaokokota dhambi kama kwa kamba za mkokoteni.

19. Wanasema:“Mwache Mwenyezi-Mungu afanye haraka,tunataka kuyaona aliyosema atayafanya!Mtakatifu wa Israeli na atimize kusudi lake.Hebu na tuone ana mipango gani!”

20. Ole wao wanaosema uovu ni wemana wema ni uovu.Giza wanasema ni mwangana mwanga wanasema ni giza.Kichungu wanasema ni kitamuna kitamu wanakiona kuwa kichungu.

21. Ole wao wanaojiona kuwa wenye hekimaambao wanajiona kuwa wenye akili.

22. Ole wao mabingwa wa kunywa divai,hodari sana wa kuchanganya vileo.

23. Kwa hongo kidogo wanawaachilia wenye hatiana kuwanyima wasio na hatia haki yao.

Kusoma sura kamili Isaya 5