Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 5:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Nitaimba juu ya rafiki yangu,wimbo wa rafiki yangu na shamba lake la mizabibu:Rafiki yangu alikuwa na shamba la mizabibujuu ya kilima chenye rutuba nyingi.

2. Alililima vizuri na kuondoa mawe yote,akaotesha humo mizabibu iliyochaguliwa;alijenga mnara wa ulinzi katikati yake,akachimba kisima cha kusindikia divai.Kisha akangojea lizae zabibu,lakini likazaa zabibu chungu.

3. Kwa hiyo rafiki yangu anasema hivi:“Enyi wakazi wa Yerusalemu na watu wa Yuda,amueni tafadhali kati yangu na shamba langu.

4. Ni kitu gani nilichokosa kulifanyia shamba langu?Na nilipotazamia lizae zabibu nzuri,mbona basi, likazaa zabibu chungu?

5. “Na sasa nitawaambieninitakavyolifanya hilo shamba langu.Nitauondoa ua wake,nalo litaharibiwa.Nitaubomoa ukuta wake,nalo litakanyagwakanyagwa.

6. Nitaliacha liharibiwe kabisa,mizabibu yake haitapogolewa wala kupaliliwa.Litaota mbigili na miiba.Tena nitayaamuru mawinguyasinyeshe mvua juu yake.”

7. Naam! Shamba la mizabibu la Mwenyezi-Mungu wa majeshini jumuiya ya Waisraeli,na mizabibu mizuri aliyoipanda ni watu wa Yuda.Yeye alitazamia watende haki,badala yake wakafanya mauaji;alitazamia uadilifu,badala yake wakasababisha kilio!

8. Ole wao wanaonunua nyumba baada ya nyumba,wanaoongeza mashamba juu ya mashamba yao,mpaka kila sehemu inakuwa mali yao,na hamna nafasi kwa wengine nchini.

9. Nimemsikia Mwenyezi-Mungu wa majeshi akitamka hivi:“Hakika nyumba nyingi zitabaki tupu,majumba makubwa mazuri bila wakazi.

10. Shamba la mizabibu la eka kumilitatoa lita nane tu za divai;anayepanda kilo 100 za mbeguatavuna kilo 10 tu za nafaka.”

11. Ole wao wanaoamka asubuhi na mapemawapate kukimbilia kunywa kileo;wanaokesha hata usiku,mpaka divai iwaleweshe!

12. Katika karamu zao, hapakosekani vinubi,zeze, matari, filimbi na divai.Lakini hawajali matendo ya Mwenyezi-Mungu,wala kuzitambua kazi za mikono yake.

Kusoma sura kamili Isaya 5