Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 49:19-26 Biblia Habari Njema (BHN)

19. “Kweli umekumbana na uharibifu,makao yako yamekuwa matupu,na nchi yako imeteketezwa.Lakini sasa itakuwa ndogo mno kwa wakazi wake;na wale waliokumaliza watakuwa mbali.

20. Wanao waliozaliwa uhamishoni,watakulalamikia wakisema:‘Nchi hii ni ndogo mno;tupatie nafasi zaidi ya kuishi.’

21. Hapo ndipo utakapojiuliza mwenyewe:‘Nani aliyenizalia watoto wote hawa?Nilifiwa na wanangu bila kupata wengine.Nilipelekwa uhamishoni na kutupwa mbali;nani basi aliyewalea watoto hawa?Mimi niliachwa peke yangu,sasa, hawa wametoka wapi?’”

22. Bwana Mungu asema hivi:“Nitayapungia mkono mataifa;naam, nitayapa ishara,nayo yatawabeba watoto wenu wa kiume,kadhalika na watoto wenu wa kikena kuwarudisha kwako.

23. Wafalme watakushughulikia,na malkia watakutengenezea chakula.Watakusujudia na kukupa heshima,na kuramba vumbi iliyo miguuni pako.Hapo utatambua kuwa mimi ni Mwenyezi-Mungu;wote wanaonitegemea hawataaibika.”

24. Watu wa Yerusalemu walalamika:“Je, shujaa aweza kunyanganywa nyara zake?Au mateka wa mtu katili waweza kuokolewa?”

25. Mwenyezi-Mungu ajibu:“Naam! Hata nyara za shujaa zitachukuliwa,mateka wa mtu katili wataokolewa.Mimi mwenyewe nitawakabili maadui zako,mimi mwenyewe nitawaokoa watoto wako.

26. Nitawafanya wanaokukandamiza watafunane;watalewa damu yao wenyewe kama divai.Hapo binadamu wote watatambua kwambamimi ni Mwenyezi-Mungu, Mwokozi wako,mimi ni Mkombozi wako, Mwenye Nguvu wa Yakobo.”

Kusoma sura kamili Isaya 49