Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 48:18-22 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Laiti ungalizitii amri zangu!Hapo baraka zingekutiririkia kama mto,ungepata fanaka kwa wingi kama mawimbi ya bahari.

19. Wazawa wako wangekuwa wengi kama mchanga,naam, wangekuwa wengi kama chembe za mchanga.Jina lao kamwe lisingaliondolewa,kumbukumbu lao halingalitoweka mbele yangu.”

20. Sasa, ondokeni Babuloni!Kimbieni kutoka Kaldayo!Tangazeni jambo hili kwa sauti za shangwe,enezeni habari zake kila mahali duniani.Semeni: “Mwenyezi-Mungu amelikomboataifa la mtumishi wake Yakobo.”

21. Alipowaongoza jangwani hawakuona kiu,aliwatiririshia maji kutoka mwambani,aliupasua mwamba maji yakabubujika.

22. Lakini Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu waovu sitawapa amani.”

Kusoma sura kamili Isaya 48