Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 47:11-15 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Lakini maafa yatakupataambayo hutaweza kujiepusha nayo.Balaa litakukumbaambalo hutaweza kulipinga;maangamizi yatakujia ghaflaambayo hujapata kamwe kuyaona.

12. Endelea basi na uganga wako,tegemea wingi wa uchawi wako.Wewe uliyapania hayo tangu ujana wakoukitumainia kwamba utafanikiwaau kusababisha kitisho kwa watu!

13. Wewe umejichosha bure na washauri wako.Basi, na wajitokeze hao wanajimu wakuokoe!Wao huzigawa mbingu sehemusehemu,huzichunguza nyotana kubashiri kila mwezi yatakayokupata.

14. “Kumbuka, wao ni kama mabua makavu:Moto utayateketezea mbali!Hawawezi hata kujiokoa wenyewembali na ukali wa moto huo.Moto huo si wa kujipatia joto,huo si moto wa kuota!

15. Ndivyo watakavyokuwa hao uliowategemea hivyo,hao uliojishughulisha nao tangu ujana wako.Watatangatanga kila mmoja njia yake;hakuna hata mmoja atakayeweza kukuokoa.”

Kusoma sura kamili Isaya 47