Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 47:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Teremka uketi mavumbiniewe Babuloni binti mzuri!Keti chini pasipo kiti cha enziewe binti wa Wakaldayo!Tokea sasa hutaitwa tena mwororo wala nadhifu.

2. Twaa mawe ya kusagia, usage unga kama mtumwa!Vua utaji wako, ukavue na mavazi yako!Pandishia vazi lako miguuni, ukavuke mito.

3. Watu watauona uchi wako;naam, wataiona aibu yako.Mimi nitalipiza kisasi,wala sitamhurumia yeyote.”

4. Mkombozi wetu ndiye Mtakatifu wa Israeli;Mwenyezi-Mungu wa majeshi ndilo jina lake.

Kusoma sura kamili Isaya 47