Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 45:4-10 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Kwa ajili ya mtumishi wangu Yakobo,naam, kwa ajili ya mteule wangu Israeli,nimekuita kwa jina lako;nimekupa jina la heshima ingawa wewe hunijui.

5. “Mimi ni Mwenyezi-Mungu, wala hakuna mwingine;hakuna Mungu mwingine ila mimi.Ninakuimarisha ingawa wewe hunijui,

6. ili watu wote, toka mashariki hadi magharibi,wajue kwamba hakuna Mungu mwingine ila mimi;mimi ni Mwenyezi-Mungu na hakuna mwingine.

7. Mimi hufanya mwanga na kuumba giza;huleta fanaka na kusababisha balaa.Mimi Mwenyezi-Mungu hutenda vitu hivi vyote.

8. Enyi mbingu, nyesheni kutoka huko juu,mawingu na yadondoshe uadilifu;dunia na ifunuke, ichipushe wokovu,na kuchanusha uadilifu pia!Mimi, Mwenyezi-Mungu nimefanya hayo.”

9. Ole wake mtu ashindanaye na Muumba wake,mtu aliye chombo cha udongokushindana na mfinyanzi wake!Je, udongo humwuliza anayeufinyanga:“Unatengeneza nini hapa?”Au kumwambia, “Kazi yako si kamili!”

10. Ole wake mtoto amwambiaye baba yake,“Kwa nini umenizaa?”Au amwambiaye mama yake,“Ya nini umenileta duniani?”

Kusoma sura kamili Isaya 45