Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 45:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu asema hivi juu ya Koreshi:“Wewe ni mfalme wangu niliyekuteua;mimi naitegemeza nguvu yakoili uyashinde mataifa mbele yako,na kuzivunja nguvu za wafalme.Mimi nayafungua malango ya mji mbele yako,na hakuna lango litakalofungwa.

2. Mimi nitakutangulia,na kuisawazisha milima mbele yako.Nitaivunjavunja milango ya shaba,na kuvikatakata vizuizi vyake vya chuma.

3. Nitakupa hazina zilizofichwa gizani,na mali iliyo mahali pa siri,upate kutambua kwamba mimi ndimi Mwenyezi-Mungu,Mungu wa Israeli, ninayekuita kwa jina lako.

4. Kwa ajili ya mtumishi wangu Yakobo,naam, kwa ajili ya mteule wangu Israeli,nimekuita kwa jina lako;nimekupa jina la heshima ingawa wewe hunijui.

5. “Mimi ni Mwenyezi-Mungu, wala hakuna mwingine;hakuna Mungu mwingine ila mimi.Ninakuimarisha ingawa wewe hunijui,

Kusoma sura kamili Isaya 45