Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 43:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Mwenyezi-Mungu aliyewaumba enyi watu wa Yakobo,yeye aliyewafanya enyi watu wa Israeli, asema:“Msiogope, maana mimi nimewakomboa;nimewaita kwa jina nanyi ni wangu.

2. Mkipita katika mafuriko,mimi nitakuwa pamoja nanyi;mkipita katika mito,haitawashinda nguvu.Mkitembea katika moto,hamtaunguzwa;mwali wa moto hautawaunguza.

3. Maana mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu,Mungu Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wenu.Nitaitoa nchi ya Misri iwe fidia yenu,nitaitoa Kushi na Seba ili mwachwe huru.

4. Kwa vile mna thamani mbele yangu,kwa kuwa nimewapa hadhi na kuwapenda,mimi nawaacha watu kusudi niwapate nyinyi,nayaachilia mataifa badala ya maisha yenu.

5. Msiogope maana mimi nipo pamoja nanyi.“Nitawarudisha wazawa wenu toka mashariki,nitawakusanyeni kutoka magharibi.

6. Nitaiambia kaskazini, ‘Waache waondoke’,na kusini, ‘Usiwazuie’!Warudisheni watu kutoka mbali,kutoka kila mahali duniani.

7. Kila mmoja hujulikana kwa jina langu,niliwaumba wote na kuwafanyakwa ajili ya utukufu wangu.”

Kusoma sura kamili Isaya 43