Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 42:1-9 Biblia Habari Njema (BHN)

1. “Tazameni mtumishi wangu ninayemtegemeza;mteule wangu ambaye moyo wangu umependezwa naye.Nimeiweka roho yangu juu yake,naye atayaletea mataifa haki.

2. Hatalia wala hatapiga kelele,wala hatapaza sauti yake barabarani.

3. Mwanzi uliochubuka hatauvunja,utambi ufukao moshi hatauzima;ataleta haki kwa uaminifu.

4. Yeye hatafifia wala kufa moyo,hata atakapoimarisha haki duniani.Watu wa mbali wanangojea mwongozo wake.”

5. Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungualiyeziumba mbingu, akazitandaza kama hema,yeye aliyeiunda nchi na vyote vilivyomo,yeye awapaye watu waliomo pumzi,na kuwajalia uhai wote waishio humo:

6. “Mimi Mwenyezi-Mungu nimekuita kutenda haki,nimekushika mkono na kukulinda.Kwa njia yako nitaweka ahadi na watu wote,wewe utakuwa mwanga wa mataifa.

7. Utayafumbua macho ya vipofu,utawatoa wafungwa gerezani,waliokaa gizani utawaletea uhuru.

8. Jina langu mimi ni Mwenyezi-Mungu;utukufu wangu sitampa mwingine,wala sifa zangu sanamu za miungu.

9. Tazama, mambo niliyotabiri yametukia;na sasa natangaza mambo mapya,nakueleza hayo kabla hayajatukia.”

Kusoma sura kamili Isaya 42