1. “Tazameni mtumishi wangu ninayemtegemeza;mteule wangu ambaye moyo wangu umependezwa naye.Nimeiweka roho yangu juu yake,naye atayaletea mataifa haki.
2. Hatalia wala hatapiga kelele,wala hatapaza sauti yake barabarani.
3. Mwanzi uliochubuka hatauvunja,utambi ufukao moshi hatauzima;ataleta haki kwa uaminifu.
4. Yeye hatafifia wala kufa moyo,hata atakapoimarisha haki duniani.Watu wa mbali wanangojea mwongozo wake.”
5. Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungualiyeziumba mbingu, akazitandaza kama hema,yeye aliyeiunda nchi na vyote vilivyomo,yeye awapaye watu waliomo pumzi,na kuwajalia uhai wote waishio humo:
6. “Mimi Mwenyezi-Mungu nimekuita kutenda haki,nimekushika mkono na kukulinda.Kwa njia yako nitaweka ahadi na watu wote,wewe utakuwa mwanga wa mataifa.
7. Utayafumbua macho ya vipofu,utawatoa wafungwa gerezani,waliokaa gizani utawaletea uhuru.