Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 40:7-18 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Majani hunyauka na ua hufifia,Mwenyezi-Mungu avumishapo upepo juu yake.Hakika binadamu ni kama majani.

8. Majani hunyauka na ua hufifia,lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.”

9. Nenda juu ya mlima mrefu,ewe Siyoni, ukatangaze habari njema.Paza sauti yako kwa nguvu,ewe Yerusalemu, ukatangaze habari njema.paza sauti yako bila kuogopa.Iambie miji ya Yuda:“Mungu wenu anakuja.”

10. Bwana Mungu anakuja na nguvu,kwa mkono wake anatawala.Zawadi yake iko pamoja naye,na tuzo lake analo.

11. Atalilisha kundi lake kama mchungaji,atawakusanya wanakondoo mikononi mwake,atawabeba kifuani pake,na kondoo wanyonyeshao atawaongoza polepole.

12. Nani awezaye kupima maji ya bahari kwa konzi yake,kuzipima mbingu kwa mikono yake?Nani awezaye kuutia udongo wa dunia kikombeni;kuipima milima kwa mizaniau vilima kwa kipimo cha uzani?

13. Nani awezaye kuiongoza akili ya Mwenyezi-Mungu,au kuwa mshauri wake na kumfunza?

14. Mwenyezi-Mungu alimtaka nani shauri,ndipo akapata kuwa mwenye ujuzi?Nani aliyemfunza njia za haki?Nani aliyemfundisha maarifa,na kumwonesha namna ya kuwa na akili?

15. Kwake mataifa ni kama tone la maji katika ndoo,ni kama vumbi juu ya mizani.Kwake visiwa ni vyepesi kama vumbi laini.

16. Kuni zote za Lebanonina wanyama wake wotehavitoshi kwa sadaka ya kuteketezwa mbele yake.

17. Mataifa yote si kitu mbele yake;kwake ni vitu duni kabisa na batili.

18. Mtamlinganisha Mungu na nini basi,au ni kitu gani cha kumfananisha naye?

Kusoma sura kamili Isaya 40