Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 40:6-11 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Sikiliza! Kuna sauti inasema, “Tangaza!”Nami nikauliza, “Nitangaze nini?”Naye: “Tangaza: Binadamu wote ni kama majani;uthabiti wao ni kama ua la shambani.

7. Majani hunyauka na ua hufifia,Mwenyezi-Mungu avumishapo upepo juu yake.Hakika binadamu ni kama majani.

8. Majani hunyauka na ua hufifia,lakini neno la Mungu wetu ladumu milele.”

9. Nenda juu ya mlima mrefu,ewe Siyoni, ukatangaze habari njema.Paza sauti yako kwa nguvu,ewe Yerusalemu, ukatangaze habari njema.paza sauti yako bila kuogopa.Iambie miji ya Yuda:“Mungu wenu anakuja.”

10. Bwana Mungu anakuja na nguvu,kwa mkono wake anatawala.Zawadi yake iko pamoja naye,na tuzo lake analo.

11. Atalilisha kundi lake kama mchungaji,atawakusanya wanakondoo mikononi mwake,atawabeba kifuani pake,na kondoo wanyonyeshao atawaongoza polepole.

Kusoma sura kamili Isaya 40