Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 40:21-31 Biblia Habari Njema (BHN)

21. Je, nyinyi bado hamjui?Je, hamjapata kusikia?Je, hamkuambiwa tangu mwanzo?Je, hamjafahamu mwanzo wa dunia?

22. Dunia iliumbwa na huyo aketiye juu ya mbingu;kutoka huko wakazi wa dunia ni kama panzi!Yeye amezitandaza mbingu kama pazia,na kuzikunjua kama hema la kuishi.

23. Yeye huwaporomosha wakuu wenye nguvu,watawala wa dunia huwafanya kuwa si kitu.

24. Mara tu wanaposimikwa na kuanza kuota,hata kabla hawajatoa mizizi kama miti udongoni,Mwenyezi-Mungu akiwapulizia hunyauka,kimbunga huwapeperusha kama makapi!

25. Mungu Mtakatifu auliza hivi:“Nani basi, mtakayemlinganisha nami?Je, kuna mtu aliye kama mimi?”

26. Inueni macho yenu juu mbinguni!Je, ni nani aliyeziumba nyota hizo?Ni yule aziongozaye kama jeshi lake,anayeijua idadi yake yote,aziitaye kila moja kwa jina lake.Kwa sababu yeye ni mwenye nguvu nyingi,hakuna hata moja inayokosekana.

27. Enyi watu wa Israeli wazawa wa Yakobo,kwa nini mnalalamika na kusema:“Mwenyezi-Mungu hatujali sisi!Mungu wetu hajali haki yetu!”

28. Je, nyinyi bado hamjui?Je, hamjapata kusikia?Mwenyezi-Mungu ndiye Mungu wa milele;yeye ndiye Muumba wa kila kitu duniani.Yeye hafifii kamwe wala kuishiwa nguvu.Maarifa yake hayachunguziki.

29. Yeye huwapa uwezo walio hafifu,wanyonge huwapa nguvu.

30. Hata vijana watafifia na kulegea;naam, wataanguka kwa uchovu.

31. Lakini wote wanaomtumainia Mwenyezi-Mungu,watapata nguvu mpya.Watapanda juu kwa mabawa kama tai;watakimbia bila kuchoka;watatembea bila kulegea.

Kusoma sura kamili Isaya 40