Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 32:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kutatokea mfalme atakayetawala kwa uadilifu,nao viongozi wataongoza kwa kufuata haki.

2. Kila mmoja atakuwa kama mahali pa kujikinga na upepo,kama mahali pa kujificha wakati wa tufani.Watakuwa kama vijito vya maji katika nchi kame,kama kivuli cha mwamba mkubwa jangwani.

3. Macho hayatafumbwa tena,masikio yatabaki wazi.

4. Wafanyao mambo kwa hamaki wataamua kwa busara,wenye kigugumizi wataongea sawasawa.

5. Wapumbavu hawataitwa tena waungwana,wala walaghai hawataitwa tena waheshimiwa.

6. Wapumbavu hunena upumbavu,na fikira zao hupanga kutenda uovu,kutenda mambo yasiyo mema,kusema mambo ya kumkufuru Mwenyezi-Mungu.Huwaacha wenye njaa bila chakula,na wenye kiu huwanyima kinywaji.

7. Ulaghai wa walaghai ni mbaya;hao huzua visa viovu,na kumwangamiza maskini kwa maneno ya uongo,hata kama madai ya maskini ni halali.

8. Lakini waungwana hutenda kiungwana,nao hutetea mambo ya kiungwana.

9. Inukeni, enyi wanawake mnaostarehe, mnisikilize;sikilizeni ninayosema enyi mabinti mlioridhika.

10. Katika mwaka mmoja hivi mtatetemeka nyinyi mliotosheka;maana hamtapata mavuno yoyote,na mavuno ya zabibu yatatoweka.

11. Tetemekeni kwa woga, enyi mnaojikalia tu;tetemekeni kwa hofu, enyi mnaostarehe!Vueni nguo zenu, mbaki uchi,mjifunge vazi la gunia viunoni mwenu.

12. Jipigeni vifua kwa huzuni,ombolezeni, kwa sababu ya bustani zilizokuwa nzuri,kwa mizabibu iliyokuwa ikizaa sana,

Kusoma sura kamili Isaya 32