Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 31:3-9 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Wamisri ni binadamu tu wala si Mungu;farasi wao nao ni wanyama tu, si roho.Mwenyezi-Mungu akiunyosha mkono wake,taifa linalotoa msaada litajikwaa,na lile linalosaidiwa litaanguka;yote mawili yataangamia pamoja.

4. Mwenyezi-Mungu aliniambia:“Kama vile simba au mwanasimba angurumavyokuyakinga mawindo yake,hata kundi la wachungaji likiitwa kumkabili,yeye hatishiki kwa kelele zao,wala hashtuki kwa sauti zao.Ndivyo atakavyoshuka Mwenyezi-Mungu wa majeshikupigana juu ya mlima Siyoni na kilima chake.

5. Kama ndege arukavyo juu ya viota vyake,ndivyo Mwenyezi-Mungu atakavyoulinda Yerusalemu,ataulinda na kuukomboa,atauhifadhi na kuuokoa.

6. Enyi Waisraeli,mrudieni huyo mliyemsaliti vibaya.

7. Wakati utafika ambapo nyotemtavitupilia mbali vinyago vyenuvya fedha na dhahabu ambavyommejitengenezea kwa mikono yenu,vikawakosesha.

8. Hapo Waashuru watauawa kwa upanga,lakini si kwa upanga wa binadamu;naam, wataangamizwa kwa upangaambao ni zaidi ya ule wa binadamu.Waashuru watakimbiana vijana wao watafanyizwa kazi za kitumwa.

9. Mfalme wao atatoroka kwa hofu,na maofisa wao wataiacha bendera yao kwa woga.Hayo ameyatamka Mwenyezi-Munguambaye moto wake umo mjini Siyoni,naam, tanuri lake limo mjini Yerusalemu.”

Kusoma sura kamili Isaya 31