Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 30:9-18 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Watu hawa ni waasi, watoto wasioaminika;watu wasiopenda kusikia mafunzo ya Mwenyezi-Mungu.

10. Huwaambia waonaji: ‘Msione maono’,na manabii: ‘Msitutangazie ukweli,bali tuambieni mambo ya kupendeza,toeni unabii wa mambo ya udanganyifu tu.

11. Geukeni na kuiacha njia ya ukweli;msituambie tena juu ya Mungu, Mtakatifu wa Israeli.’”

12. Kwa hiyo Mungu, Mtakatifu wa Israeli asema:“Nyinyi mmeukataa ujumbe wangu;mkapania kufanya dhuluma na udanganyifu.

13. Basi, dhambi hii itawaleteeni maangamizikama ufa mkubwa katika ukuta mrefu;utabomoka mara na kuanguka chini ghafla.

14. Kuporomoka kwa ukuta huo,ni kama kupasuka kwa chunguambacho kimepasuliwa vibaya sana,bila kusalia kigae cha kuchukulia moto mekoni,au kuchotea maji kisimani.”

15. Bwana Mungu, Mtakatifu wa Israeli, asema:“Mkinirudia na kutulia mtaokolewa;kwa utulivu na kunitumainia mtapata nguvu.”Lakini nyinyi hamkutaka.

16. Badala yake mlisema,“La! Sisi tutakimbia na farasi wenye mbio.”Sawa, mtakimbia na farasi wenye mbio,lakini farasi wa maadui zenu wana mbio zaidi.

17. Watu wenu elfu moja watamkimbia askari mmoja adui;na askari watano maadui watawakimbizeni nyote.Mwishowe, watakaosaliawatakuwa kama mlingoti wa bendera mlimani,kama alama iliyo juu ya kilima.

18. Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu anangoja awafadhili,atainuka na kuwaonea huruma.Maana, Mwenyezi-Mungu ni Mungu atendaye haki.Heri wote wale wanaomtumainia.

Kusoma sura kamili Isaya 30