Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 30:23-30 Biblia Habari Njema (BHN)

23. Mtakapopanda mbegu zenu, Mwenyezi-Mungu atanyesha mvua kwa wakati wake, nazo zitakua na kuwapa mavuno mengi. Mifugo yenu nayo itapata malisho kwa wingi.

24. Mafahali na punda wenu wa kulimia watapata malisho yaliyochambuliwa vizuri na kutiwa chumvi.

25. Wakati utakapofika ambapo maadui watauawa na ngome zao kubomolewa, vijito vya maji vitatiririka kutoka kila mlima na kilima.

26. Tena mwezi utawaka kama jua, nao mwanga wa jua utakuwa mara saba ya mwanga wake wa kawaida, kana kwamba mwanga wa siku saba umeangaza katika siku moja. Mambo haya yote yatatukia wakati Mwenyezi-Mungu atakapoyafunga na kuyaponya majeraha aliyowaletea watu wake.

27. Tazameni, Mwenyezi-Mungu mwenyewe anakuja toka mbali!Amewaka hasira na moshi wafuka;midomo yake yaonesha ghadhabu yake,maneno anayosema ni kama moto uteketezao.

28. Pumzi yake ni kama mafuriko ya mtoambao maji yake yanafika hadi shingoni.Anakuja kuyachekecha mataifa kwa chekecheke ya maangamizi,kuwafunga lijamu na kuwapeleka wasikotaka.

29. Lakini nyinyi watu wa Yerusalemu mtaimba kwa furaha kama mfanyavyo wakati wa mkesha wa sikukuu. Mtajaa furaha kama watu wanaotembea kwa mdundo wa muziki wa filimbi kwenda mlimani kwa Mwenyezi-Mungu, Mwamba wa Israeli.

30. Mwenyezi-Mungu atawafanya watu wote waisikie sauti yake tukufu na pigo la nguvu yake lionekane kwa hasira nyingi. Kutakuwa na ndimi za moto mkali, ngurumo, dhoruba na mvua ya mawe.

Kusoma sura kamili Isaya 30