Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 29:8-16 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Mataifa yote yanayoushambulia mji wa Yerusalemuyatakuwa kama mtu mwenye njaa anayeota anakulalakini aamkapo bado anaumwa na njaa!Au mtu mwenye kiu anayeota kuwa anakunywa,lakini anaamka mdhaifu, bado ana kiu.

9. Endeleeni kuwa wapumbavu na kuduwaa!Jipofusheni na kuwa vipofu!Leweni lakini si kwa divai;pepesukeni lakini si kwa pombe.

10. Mwenyezi-Mungu amewamiminia hali ya usingizi mzito;ameyafumba macho yenu enyi manabii,amefunika vichwa vyenu enyi waonaji.

11. Basi, kwenu nyinyi maono yote haya ni kama ujumbe ulioandikwa katika kitabu kilichofungwa kwa mhuri. Ukimpelekea mtu yeyote ajuaye kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atasema, “Siwezi kukisoma kwani kimefungwa kwa mhuri.”

12. Na ukimpa mtu yeyote asiyejua kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atakuambia, “Sijui kusoma.”

13. Bwana asema,“Watu hawa huja kuniabudu kwa maneno matupu,hali mioyo yao iko mbali nami.Wananiheshimu kulingana na mapokeo ya watu tu,jambo walilojifunza wao wenyewe.

14. Hivyo, nitawatenda tena watu hawa maajabu,mambo ya ajabu na ya kushangaza.Nao wenye hekima wao wataishiwa hekima,na busara ya wenye busara wao itatoweka.

15. “Ole mnaomficha Mwenyezi-Mungu mipango yenu,mnaotenda matendo yenu gizanina kusema: ‘Hamna atakayetuona;nani awezaye kujua tunachofanya?’

16. Nyinyi mnafanya mambo kinyume kabisa!Je, mfinyanzi na udongo ni hali moja?Chombo hakiwezi kumwambia aliyekitengeneza:‘Wewe hukunitengeneza.’Kilichofinyangwa hakiwezi kumwambia aliyekiumba,‘Wewe hujui chochote.’”

Kusoma sura kamili Isaya 29