Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 29:6-12 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Mwenyezi-Mungu wa majeshi atakuja kukusaidia;atakuja na ngurumo, tetemeko la ardhi na sauti kubwa;atakuja na kimbunga, tufani na moto uunguzao.

7. Hapo, kundi la mataifa yote yanayoshambulia Yerusalemu,wote wanaoshambulia ngome yake na kuutia wasiwasi,watatoweka kama ndoto, kama maono ya usiku.

8. Mataifa yote yanayoushambulia mji wa Yerusalemuyatakuwa kama mtu mwenye njaa anayeota anakulalakini aamkapo bado anaumwa na njaa!Au mtu mwenye kiu anayeota kuwa anakunywa,lakini anaamka mdhaifu, bado ana kiu.

9. Endeleeni kuwa wapumbavu na kuduwaa!Jipofusheni na kuwa vipofu!Leweni lakini si kwa divai;pepesukeni lakini si kwa pombe.

10. Mwenyezi-Mungu amewamiminia hali ya usingizi mzito;ameyafumba macho yenu enyi manabii,amefunika vichwa vyenu enyi waonaji.

11. Basi, kwenu nyinyi maono yote haya ni kama ujumbe ulioandikwa katika kitabu kilichofungwa kwa mhuri. Ukimpelekea mtu yeyote ajuaye kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atasema, “Siwezi kukisoma kwani kimefungwa kwa mhuri.”

12. Na ukimpa mtu yeyote asiyejua kusoma, ukamwambia, “Hebu nisomee kitabu hiki,” atakuambia, “Sijui kusoma.”

Kusoma sura kamili Isaya 29