Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 29:21-24 Biblia Habari Njema (BHN)

21. Watatoweka wale wanaopotosha kesi ya mtu mahakamani,watu wanaowafanyia hila mahakimuna wasemao uongo kuwanyima haki yao wasio na hatia.

22. Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu aliyemkomboa Abrahamu,asema hivi kuhusu wazawa wa Yakobo:“Wazawa wa Yakobo hawataaibishwa tena,hawatainamisha vichwa vyao tena kwa aibu.

23. Watakapowaona watoto wao,watoto niliowajalia mimi mwenyewe,watalitukuza jina langu mimi Mtakatifu wa Yakobo;watakuwa na uchaji kwangu mimi Mungu wa Israeli.

24. Waliopotoka rohoni watapata maarifana wenye kununa watakubali kufunzwa.”

Kusoma sura kamili Isaya 29