Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 29:19-24 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Wanyofu watapata furaha mpya kwa Mwenyezi-Mungu,na maskini wa watu watashangilia kwa furahakwa sababu ya Mungu, Mtakatifu wa Israeli.

20. Majitu makatili yataangamizwa,wenye kumdhihaki Mungu watakwisha,wote wanaootea kutenda maovu watatokomezwa.

21. Watatoweka wale wanaopotosha kesi ya mtu mahakamani,watu wanaowafanyia hila mahakimuna wasemao uongo kuwanyima haki yao wasio na hatia.

22. Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu aliyemkomboa Abrahamu,asema hivi kuhusu wazawa wa Yakobo:“Wazawa wa Yakobo hawataaibishwa tena,hawatainamisha vichwa vyao tena kwa aibu.

23. Watakapowaona watoto wao,watoto niliowajalia mimi mwenyewe,watalitukuza jina langu mimi Mtakatifu wa Yakobo;watakuwa na uchaji kwangu mimi Mungu wa Israeli.

24. Waliopotoka rohoni watapata maarifana wenye kununa watakubali kufunzwa.”

Kusoma sura kamili Isaya 29