Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 29:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Ole wako Yerusalemu, madhabahu ya Mungu;mji ambamo Daudi alipiga kambi yake!Miaka yaja na kupita,na sikukuu zako zaendelea kufanyika;

2. lakini mimi Mungu nitauhuzunisha Yerusalemu,nako kutakuwa na vilio na maombolezo,mji wenyewe utakuwa kama madhabahuiliyolowa damu ya watu waliouawa.

3. Mimi nitapanga jeshi dhidi ya Yerusalemu,nami nitauzingira na kuushambulia.

4. Utaangushwa mbali sana ndani ya ardhi;kutoka huko mbali utatoa sauti;maneno yako yatatoka huko chini mavumbini;sauti yako itatoka ardhini kama ya mzimu.

5. Kundi la maadui zako litakuwa kama vumbi laini,waliokutendea ukatili watakuwa kama makapi.Hayo yatafanyika ghafla.

6. Mwenyezi-Mungu wa majeshi atakuja kukusaidia;atakuja na ngurumo, tetemeko la ardhi na sauti kubwa;atakuja na kimbunga, tufani na moto uunguzao.

7. Hapo, kundi la mataifa yote yanayoshambulia Yerusalemu,wote wanaoshambulia ngome yake na kuutia wasiwasi,watatoweka kama ndoto, kama maono ya usiku.

Kusoma sura kamili Isaya 29