Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 28:14-26 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Basi, sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu,enyi wenye madharau mnaotawala watu wa Yerusalemu,

15. “Nyinyi mnajidai mmefanya mkataba na kifo,mmefanya mapatano na Kuzimu!Nyinyi mwasema eti balaa lijapo halitawapata,kwa sababu mmefanya uongo kuwa tegemeo lenu,na udanganyifu kuwa kinga yenu!”

16. Basi, hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi-Mungu:“Tazama! Naweka mjini Siyoni jiwe la msingi,jiwe ambalo limethibitika.Jiwe la pembeni, la thamani,jiwe ambalo ni la msingi thabiti;jiwe lililo na maandishi haya:‘Anayeamini hatatishika.’

17. Nitatumia haki kama kipimo changu,nitatumia uadilifu kupimia.”Mvua ya mawe itaufagilia mbali uongo mnaoutegemea,na mafuriko yataharibu kinga yenu.

18. Hapo mkataba wenu na kifo utabatilishwa,na mapatano yenu na Kuzimu yatafutwa.Janga lile kuu litakapokujalitawaangusheni chini.

19. Kila litakapopitia kwenu litawakumba;nalo litapita kila asubuhi, mchana na usiku.Kusikia ujumbe huu tu kutakuwa kitisho.

20. Kwenu itakuwa kama ajinyoshaye juu ya kitanda kifupi mno,au kujifunika kwa blanketi lililo dogo mno!

21. Maana Mwenyezi-Mungu atainuka kama kule mlimani Perazimu;atawaka hasira kama kule bondeni Gibeoni.Atatekeleza mpango wake wa ajabu;atatenda kazi yake ya kustaajabisha.

22. Basi, nyinyi msiwe na madharauvifungo vyenu visije vikakazwa zaidi.Maana nimesikia kuwa Mwenyezi-Mungu wa majeshiameazimia kuiangamiza nchi yote.

23. Tegeni sikio msikilize ninayowaambieni;sikilizeni kwa makini hotuba yangu.

24. Je, alimaye ili kupanda hulima tu?Je, huendelea kulima na kusawazisha shamba lake?

25. La! Akisha lisawazisha shamba lake,hupanda mbegu za bizari na jira,akapanda ngano na shayiri katika safu,na mipakani mwa shamba mimea mingineyo.

26. Mtu huyo huwa anajua la kufanya,kwa sababu Mungu wake humfundisha.

Kusoma sura kamili Isaya 28