Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 26:18-21 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Sisi tulipata maumivu ya kujifungualakini tukajifungua tu upepo!Hatukupata ushindi wowote kwa ajili ya nchi yetu,hatukuweza kuongeza idadi ya watu katika nchi.

19. Wafu wako wataishi tena,miili yao itafufuka.Wanaolala mavumbini wataamka na kuimba kwa furaha!Mungu atapeleka umande wake wa uhai,nao walio kwa wafu watatoka hai.

20. Njoni watu wangu, ingieni majumbani mwenu,mkajifungie humo ndani.Jificheni kwa muda mfupi,mpaka ifike ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu.

21. Maana Mwenyezi-Mungu aja kutoka kwake juu,kutoka makao yake huko mbinguni;kuwaadhibu wakazi wa dunia kwa uovu wao.Nayo dunia haitaficha tena wale waliouawa,ila itaufichua umwagaji damu wote.

Kusoma sura kamili Isaya 26