Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 23:8-18 Biblia Habari Njema (BHN)

8. Ni nani aliyepanga mambo haya dhidi ya Tiro,mji uliowatawaza wafalme,wafanyabiashara wake walikuwa wakuu,wakaheshimiwa duniani kote?

9. Ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi!Yeye ndiye aliyeyapanga haya yote.Alifanya hivyo akiharibu kiburi chaona kuwaaibisha waheshimiwa wake.

10. Limeni sasa ardhi yenu enyi wakazi wa Tarshishi;maana hamna tena bandari kwa ajili ya meli kubwa.

11. Mwenyezi-Mungu ameunyosha mkono wake juu ya bahari,amezitetemesha falme;ametoa amri kuziharibu ngome za Kanaani.

12. Alisema: “Ewe binti Sidonihutaweza kufanya sherehe tena;hata ukikimbilia Kupro,huko nako hutapata pumziko!”

13. (Ni Wakaldayo, wala si Waashuru, waliowaacha wanyama wa porini wauvamie mji wa Tiro. Wao ndio waliouzungushia mji huo minara ya kuushambulia, wakayabomoa majumba yake na kuufanya magofu.)

14. Pigeni yowe enyi meli za Tarshishi,maana kimbilio lenu limeharibiwa.

15. Hapo mji wa Tiro utasahaulika kwa muda wa miaka sabini, muda wa maisha ya mfalme. Baada ya miaka hiyo sabini, mji wa Tiro utakumbwa na kile watu wanachoimba juu ya malaya:

16. “Twaa kinubi chakouzungukezunguke mjini,ewe malaya uliyesahaulika!Imba nyimbo tamutamu.Imba nyimbo nyinginyingiili upate kukumbukwa tena.”

17. Baada ya miaka hiyo sabini, Mwenyezi-Mungu atauadhibu mji wa Tiro, nao utarudia kufanya uzinzi kwa kujiuza kwa mataifa yote ya dunia.

18. Fedha utakayopata itawekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu. Mji wenyewe hautafaidika kwa fedha hiyo ila wale wanaomwabudu Mwenyezi-Mungu wataitumia kununulia chakula kingi na mavazi mazuri.

Kusoma sura kamili Isaya 23