Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 22:9-20 Biblia Habari Njema (BHN)

9. mkaona kwamba nyufa za kuta za mji wa Daudi ni nyingi, mkajaza maji bwawa la chini.

10. Mlizikagua nyumba za mji wa Yerusalemu, mkabomoa baadhi yake ili kupata mawe ya kuimarisha kuta za mji.

11. Katikati ya kuta hizo mlijijengea birika la kuhifadhia maji yanapotiririka kutoka bwawa la zamani. Lakini hamkumtafuta Mungu aliyepanga mambo haya yote; hamkumjali yeye aliyepanga hayo yote tangu zamani.

12. Siku hiyo, Mwenyezi-Mungu, wa majeshialiwataka mlie na kuomboleza,mnyoe nywele na kuvaa mavazi ya gunia.

13. Lakini nyinyi mkafurahi na kusherehekea.Mlichinja ng'ombe na kondoo,mkala nyama na kunywa divai.Nyinyi mlisema:“Acha tule na kunywamaana kesho tutakufa.”

14. Mwenyezi-Mungu wa majeshi alinifunulia haya akisema:“Hakika hawatasamehewa uovu huu,watakufa bila kusamehewa.Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.”

15. Mwenyezi-Mungu wa majeshi aliniambia niende kwa Shebna, msimamizi wa jamaa ya kifalme, nikamwambie hivi:

16. “Una haki gani kuwa huku? Je, una ndugu yeyote hapa, hata ukajichongea kaburi mwambani juu ya mlima?

17. Wewe ni mwenye nguvu, lakini Mwenyezi-Mungu atakutupilia mbali kwa nguvu.

18. Atakubana kabisa na kukuzungushazungusha, kisha atakutupa kama mpira mpaka katika nchi pana. Huko utafia karibu na magari yako ya vita unayojivunia. Wewe ni aibu kwa nyumba ya bwana wako.

19. Mwenyezi-Mungu atakungoa madarakani mwako na kukuporomosha kutoka mahali ulipo.

20. “Siku hiyo, nitamleta mtumishi wangu Eliakimu mwana wa Hilkia.

Kusoma sura kamili Isaya 22