Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 22:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kauli ya Mungu dhidi ya Bonde la Maono.Kuna nini ee Yerusalemu?Mbona watu wote mmepanda juu ya nyumba?

2. Kwa nini mnapiga kelele za shangwe,na mji wote umechangamka na kujaa vigelegele?Watu wenu waliokufa hawakuuawa vitani,wala hawakuuawa katika mapigano.

3. Maofisa wenu wote walikimbia,wakakamatwa hata kabla ya kufyatua mshale mmoja.Watu wako wote waliopatikana walitekwa,ingawa walikuwa wamekimbilia mbali.

4. Ndiyo maana nawaambieni:Msijali chochote juu yanguniacheni nilie machozi ya uchungu.Msijisumbue kunifarijikwa ajili ya balaa walilopata watu wangu.

5. Maana leo Mwenyezi-Mungu wa majeshiametuletea mchafuko:Kushindwa na wasiwasi katika Bonde la Maono.Kuta za mji zimebomolewa,mayowe ya wakazi wake yasikika mpaka milimani.

6. Majeshi ya Elamu, pinde na mishale mikononi,walikuja wamepanda farasi na magari ya vita;nalo jeshi la Kiri lilitayarisha ngao zake.

7. Mabonde yako mazuri ewe Yerusalemu,yalijaa magari ya vita na farasi;wapandafarasi walijipanga tayari langoni mwako.

8. Ulinzi wote wa Yuda uliporomoka.Siku hiyo mlikwenda kutafuta silaha zilizokuwa zimehifadhiwa katika Nyumba ya Msitu,

9. mkaona kwamba nyufa za kuta za mji wa Daudi ni nyingi, mkajaza maji bwawa la chini.

10. Mlizikagua nyumba za mji wa Yerusalemu, mkabomoa baadhi yake ili kupata mawe ya kuimarisha kuta za mji.

Kusoma sura kamili Isaya 22