Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 21:5-15 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Chakula kimetayarishwa,shuka zimetandikwa,sasa watu wanakula na kunywa.Ghafla, sauti inasikika:“Inukeni enyi watawala!Wekeni silaha tayari!”

6. Maana Bwana aliniambia,“Nenda ukaweke mlinzi;mwambie atangaze atakachoona.

7. Akiona kikosi, wapandafarasi wawiliwawili,wapandangamia na wapandapunda,na awe macho;naam, akae macho!”

8. Kisha huyo mlinzi akapaza sauti:“Bwana, nimesimama juu ya mnara wa ulinzi mchana kutwa,nimeshika zamu usiku kucha!”

9. Tazama, kikosi kinakuja,wapandafarasi wawiliwawili.Wanasema: “Babuloni umeanguka! Umeanguka!Sanamu zote za miungu yakezimetupwa chini na kuvunjwavunjwa!”

10. Ewe Israeli, watu wangu,enyi mliotwangwa na kupurwa kama nafaka.Sasa nimewaambieni mambo niliyoyasikiakwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli.

11. Kauli ya Mungu dhidi ya Duma.Ninasikia mtu ananiita kutoka Seiri:“Mlinzi, nini kipya leo usiku?Kuna kipya chochote leo usiku?”

12. Nami mlinzi nikajibu:“Asubuhi inakuja, kadhalika na usiku;ukitaka kuuliza, uliza tu;nenda urudi tena.”

13. Kauli ya Mungu dhidi ya Arabia.Enyi misafara ya Dedani,pigeni kambi leo usiku kwenye nyika za Arabia.

14. Enyi wakazi wa nchi ya Tema,wapeni maji hao wenye kiu;wapelekeeni chakula hao wakimbizi.

15. Maana wamekimbia mapanga,mapanga yaliyochomolewa,pinde zilizovutwa na ukali wa mapigano.

Kusoma sura kamili Isaya 21