Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 21:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kauli ya Mungu dhidi ya jangwa kando ya bahari.Kama vimbunga vinavyovuma kutoka kusini,wavamizi wanakuja kutoka jangwani,kutoka katika nchi ya kutisha.

2. Nimeoneshwa maono ya kutisha,maono ya watu wa hila watendao hila,maono ya watu waangamizi wafanyao maangamizi.Pandeni juu vitani enyi Waelamu;shambulieni enyi Wamedi!Mungu atakomesha mateso yoteyaliyoletwa na Babuloni.

3. Kwa maono hayo nimeingiwa na hofu kubwa,uchungu mwingi umenikumba;kama uchungu wa mama anayejifungua.Maumivu yamenizidi hata siwezi kusikia;nimefadhaika hata siwezi kuona.

4. Moyo unanidunda na woga umenikumba.Nilitamani jioni ifikelakini ilipofika ikawa ya kutetemesha.

5. Chakula kimetayarishwa,shuka zimetandikwa,sasa watu wanakula na kunywa.Ghafla, sauti inasikika:“Inukeni enyi watawala!Wekeni silaha tayari!”

Kusoma sura kamili Isaya 21