Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 2:5-12 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Sasa, enyi wazawa wa Yakobo, njoni,tutembee katika mwanga wa Mwenyezi-Mungu.

6. Sasa, ee Mungu, umewatupa watu wako, wazawa wa Yakobo.Maana kweli wachawi wa mashariki wamejaa kati yao,wapo na wapiga ramli kama kwa Wafilisti.Wanashirikiana na watu wageni.

7. Nchi yao imejaa fedha na dhahabu,hazina yao ni kubwa kupindukia.Nchi yao imejaa farasi,magari yao ya kukokotwa hayana idadi.

8. Nchi yao imejaa vinyago vya miungu,huabudu kazi ya mikono yao,vitu walivyotengeneza wao wenyewe.

9. Kwa hiyo, kila mtu ataaibishwa na kufedheheshwa.Usiwasamehe hata kidogo, ee Mungu!

10. Ingieni katika mwamba,mkajifiche mavumbini,kuiepa hasira ya Mwenyezi-Mungu,mbali na utukufu wa enzi yake.

11. Siku yaja ambapo kiburi cha watu kitashushwa,majivuno ya kila mtu yatavunjwa;na Mwenyezi-Mungu peke yake atatukuzwa siku hiyo.

12. Naam, yaja siku ya Mwenyezi-Mungu wa majeshidhidi ya wenye kiburi na majivuno,dhidi ya wote wanaojikweza;

Kusoma sura kamili Isaya 2