Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 2:11-18 Biblia Habari Njema (BHN)

11. Siku yaja ambapo kiburi cha watu kitashushwa,majivuno ya kila mtu yatavunjwa;na Mwenyezi-Mungu peke yake atatukuzwa siku hiyo.

12. Naam, yaja siku ya Mwenyezi-Mungu wa majeshidhidi ya wenye kiburi na majivuno,dhidi ya wote wanaojikweza;

13. dhidi ya mierezi yote ya Lebanoni,ambayo ni mirefu na mizuri,dhidi ya mialoni yote nchini Bashani;

14. dhidi ya milima yote mirefu,dhidi ya vilima vyote vya juu;

15. dhidi ya minara yote mirefu,dhidi ya kuta zote za ngome;

16. dhidi ya meli zote za Tarshishi,na dhidi ya meli zote nzuri.

17. Kiburi chote cha watu kitakomeshwa,majivuno ya kila mtu yatavunjwa.Na Mwenyezi-Mungu peke yake atatukuzwa siku hiyo.

18. Vinyago vyote vya miungu vitatoweka kabisa.

Kusoma sura kamili Isaya 2