Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 17:7-14 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Siku hiyo, watu watamwangalia Muumba wao, na kuelekeza macho yao kwa huyo Mtakatifu wa Israeli.

8. Hawatazielekea tena madhabahu ambazo ni kazi za mikono yao wenyewe, wala kuzitazamia tena kazi za mikono yao wenyewe, yaani sanamu za mungu Ashera na madhabahu za kufukizia ubani.

9. Siku hiyo miji yao imara itaachwa mahame, kama miji ambayo Wahivi na Waamori waliihama walipokuwa wakiwakimbia wazawa wa Israeli. Kila kitu kitakuwa uharibifu.

10. Maana wewe Israeli umemsahau Mungu aliyekuokoa,hukumkumbuka Mwamba wa usalama wako.Kwa hiyo, hata mkipanda mimea ya Baali,na kuiweka wakfu kwa mungu wa kigeni;

11. hata mkiifanya ikue siku hiyohiyo mliyoipandana kuifanya ichanue asubuhi hiyohiyo,mavuno yenu yatatowekasiku hiyo ya balaa na maumivu yasiyoponyeka.

12. Lo! Ngurumo ya watu wengi!Wananguruma kama bahari.Lo! Mlio wa watu wa mataifa!Yanatoa mlio kama wa maji mengi.

13. Mataifa yananguruma kama ngurumo ya maji mengi,lakini Mungu atayakemea, nayo yatakimbilia mbali.Yatafukuzwa kama makapi mlimani mbele ya upepo;kama vumbi litimuliwalo na kimbunga.

14. Wakati wa jioni yanaleta hofu kuu,lakini kabla ya asubuhi yametoweka!Hilo ndilo litakalowapata wanaonyakua mali yetu,ndilo litakalowapata wanaotupora.

Kusoma sura kamili Isaya 17