Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 17:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Kauli ya Mungu dhidi ya Damasko.“Damasko utakoma kuwa mji;utakuwa rundo la magofu.

2. Mitaa yake imeachwa mahame milele.Itakuwa makao ya makundi ya wanyama,wala hakuna mtu atakayewatisha.

3. Ngome za kujihami za Efraimu zitatoweka,na utawala wa Damasko utakwisha.Waashuru ambao watabaki hai,watakuwa na fedheha kama wazawa wa Israeli.Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.

4. “Siku hiyo, fahari ya Yakobo itaporomoshwa,na unono wake ataupoteza.

5. Atakwisha kama shamba lililovunwa,atafanyiwa kama mvunaji avunavyo nafaka,atakuwa kama shamba lililovunwa bondeni Refaimu.

Kusoma sura kamili Isaya 17