Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 16:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Pelekeni wanakondoo kwa mtawala wa nchi,pelekeni kutoka Sela jangwani mpaka mlimani Siyoni.

2. Kama ndege wanavyohangaika na kurukaruka,wakiwa wamefukuzwa kutoka viota vyao,ndivyo walivyo mabinti wa Moabukwenye vivuko vya Arnoni.

3. Wamoabu wanawaambia watu wa Yuda,“Tupeni mwongozo, tuamulieni.Enezeni ulinzi wenu juu yetu,kama vile usiku uenezavyo kivuli chake.Tuficheni sisi wakimbizi;msitusaliti sisi tuliofukuzwa.

4. Wakimbizi wa Moabu waishi kwenu,muwe kimbilio lao mbali na mwangamizi.”Mdhalimu atakapokuwa ametoweka,udhalimu utakapokuwa umekoma,na wavamizi kutoweka nchini,

5. utawala adili utazinduliwa katika maskani ya Daudi,mtawala apendaye kutenda haki,na mwepesi wa kufanya yaliyo sawa;atatawala humo kwa uaminifu.

6. Watu wa Yuda wanasema hivi:“Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu,tunajua jinsi alivyojivuna mno;tumesikia juu ya majivuno, kiburi na ufidhuli wake;lakini majivuno yake hayo ni bure.”

Kusoma sura kamili Isaya 16