Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 14:6-17 Biblia Habari Njema (BHN)

6. ambao walipiga nayo watu kwa hasira bila kukoma,na kuwatawala kwa udhalimu bila huruma.

7. Sasa dunia yote ina utulivu na amani,kila mtu anaimba kwa furaha.

8. Misonobari inafurahia kuanguka kwako,nayo mierezi ya Lebanoni pamoja yasema:‘Kwa vile sasa umeangushwa,hakuna mkata miti atakayekuja dhidi yetu!’

9. “Kuzimu nako kumechangamka,ili kukulaki wakati utakapokuja.Kunaiamsha mizimu ije kukusalimuna wote waliokuwa wakuu wa dunia;huwaamsha kutoka viti vyao vya enziwote waliokuwa wafalme wa mataifa.

10. Wote kwa pamoja watakuambia:‘Nawe pia umedhoofika kama sisi!Umekuwa kama sisi wenyewe!

11. Fahari yako imeteremshwa kuzimupamoja na muziki wa vinubi vyako.Chini mabuu ndio kitanda chako,na wadudu ndio blanketi lako!’

12. “Jinsi gani ulivyoporomoshwa toka mbinguni,wewe uliyekuwa nyota angavu ya alfajiri.Jinsi gani ulivyoangushwa chini,wewe uliyeyashinda mataifa!

13. Wewe ulijisemea moyoni mwako:‘Nitapanda mpaka mbinguni;nitaweka kiti changu juu ya nyota za Mungu,nitaketi juu ya mlima wakutanapo miungu,huko mbali pande za kaskazini.

14. Nitapanda vilele vya mawingunitajifanya kuwa sawa na Mungu Mkuu.’

15. Lakini umeporomoshwa hadi kuzimu;umeshushwa chini kabisa shimoni.

16. “Watakaokuona watakukodolea macho,watakushangaa wakisema:‘Je, huyu ndiye aliyetetemesha duniana kuzitikisa falme,

17. aliyegeuza dunia kuwa kama jangwa,akaangamiza miji yake,na kuwanyima wafungwa wake kurudi kwao?’

Kusoma sura kamili Isaya 14