Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 14:13-27 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Wewe ulijisemea moyoni mwako:‘Nitapanda mpaka mbinguni;nitaweka kiti changu juu ya nyota za Mungu,nitaketi juu ya mlima wakutanapo miungu,huko mbali pande za kaskazini.

14. Nitapanda vilele vya mawingunitajifanya kuwa sawa na Mungu Mkuu.’

15. Lakini umeporomoshwa hadi kuzimu;umeshushwa chini kabisa shimoni.

16. “Watakaokuona watakukodolea macho,watakushangaa wakisema:‘Je, huyu ndiye aliyetetemesha duniana kuzitikisa falme,

17. aliyegeuza dunia kuwa kama jangwa,akaangamiza miji yake,na kuwanyima wafungwa wake kurudi kwao?’

18. Wafalme wote wa mataifa wamezikwa kwa heshimakila mmoja ndani ya kaburi lake.

19. Lakini wewe umetupwa nje ya kaburi lako;kama mtoto wa kuchukiza aliyezaliwa mfumaiti yako imekanyagwakanyagwa,umerundikiwa maiti za waliouawa kwa upanga,waliotupwa mashimoni penye mawe.

20. Lakini wewe hutaunganishwa nao katika mazishi,maana uliiharibu nchi yako,wewe uliwaua watu wako.Wazawa wa waovu na wasahaulike kabisa!

21. Kaeni tayari kuwachinja watoto wakekwa sababu ya makosa ya baba zao,wasije wakaamka na kuimiliki nchi,na kuijaza dunia yote miji yao.”

22. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Nitaushambulia mji wa Babuloni na kuuangamiza kabisa. Nitaharibu kila kitu, mji wote, watoto na yeyote aliyebaki hai. Mimi Mwenyezi-Mungu nimenena.

23. Nitaufanya kuwa makao ya nungunungu, na utakuwa madimbwi ya maji. Nami nitaufagilia mbali kwa ufagio wa maangamizi. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.”

24. Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameapa:“Kama nilivyopanga,ndivyo itakavyokuwa;kama nilivyokusudia,ndivyo itakavyokamilika.

25. Nitauvunja uwezo wa Waashuru nchini mwangu;nitawakanyagakanyaga katika milima yangu.Nitawaondolea watu wangu nira ya dhuluma yao,na mzigo wa mateso yao.”

26. Huu ndio uamuzi wake Mwenyezi-Mungukuhusu dunia yote;hii ndiyo adhabu atakayotoajuu ya mataifa yote.

27. Kama Mwenyezi-Mungu wa majeshi ameamua,nani atakayeweza kubatilisha uamuzi wake?Kama amepania kutoa adhabu,ni nani atakayempinga?

Kusoma sura kamili Isaya 14