Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 10:26-34 Biblia Habari Njema (BHN)

26. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi na nitawachapa kama nilivyowachapa Wamidiani kwenye jabali la Orebu. Nitanyosha fimbo yangu juu ya bahari kuwachapa kama nilivyowafanya Wamisri.

27. Wakati huo, mzigo waliowabebesha nitauondoa na nira waliyowatia shingoni mwenu itavunjwa.”Adui amepanda kutoka Rimoni,

28. amefika mjini Ayathi.Amepitia huko Migroni,mizigo yake ameiacha Mikmashi.

29. Amekwisha pita kivukoni,usiku huu analala Geba.Watu wa Rama wanatetemeka kwa hofu,wakazi wa Gibea, mji wa Shauli, wamekimbia.

30. Pazeni sauti enyi watu wa Galimu!Tegeni sikio enyi watu wa Laisha!Jibuni enyi wenyeji wa Anathothi!

31. Watu wa Madmena wako mbioni,wakazi wa Gebimu wanakimbilia usalama.

32. Leo hii, adui atatua Nobu,atatikisa ngumi yake dhidi ya mlima Siyoni;naam, atautikisia ngumi mji wa Yerusalemu.

33. Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshiatakata matawi yake kwa ukatili;miti mirefu itaangushwa chini,walio juu wataaibishwa.

34. Atakata vichaka vya msituni kwa shoka,Lebanoni na mierezi yake maarufu itaanguka.

Kusoma sura kamili Isaya 10