Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 1:3-15 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Ngombe humfahamu mwenyewe,punda hujua kibanda cha bwana wake;lakini Waisraeli hawajui,watu wangu, hawaelewi!”

4. Ole wako wewe taifa lenye dhambi,watu waliolemewa na uovu,wazawa wa wenye kutenda maovu,watu waishio kwa udanganyifu!Nyinyi mmemwacha Mwenyezi-Mungu,mmemdharau Mtakatifu wa Israeli,mmefarakana naye na kurudi nyuma.

5. Kwa nini huachi uasi wako?Mbona wataka kuadhibiwa bado?Kichwa chote ni majeraha matupu,na moyo wote unaugua!

6. Toka wayo hadi kichwa hamna penye nafuu,umejaa majeraha na vidonda vitoavyo damu,navyo havikuoshwa, kufungwa wala kutiwa mafuta.

7. Nchi yenu imeharibiwa kabisa;miji yenu imeteketezwa kwa moto.Wageni wananyakua nchi yenu mkiona kwa macho,imeharibiwa kama uharibifu wa Sodoma.

8. Mji Siyoni umeachwa kama kibanda shambani,kama kitalu katika shamba la matango,kama mji uliozingirwa.

9. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asingalituachia wachache,tungalikwisha kuwa kama watu wa Sodoma,tungalikuwa hali ileile ya Gomora.

10. Sikilizeni neno la Mwenyezi-Munguenyi watawala waovu kama wa Sodoma!Sikilizeni mafunzo ya Mungu wetuenyi watu waovu kama wa Gomora!

11. Mwenyezi-Mungu asema hivi;“Wingi wa tambiko zenu ni kitu gani kwangu?Nimezichoka sadaka zenu za kondoo wa kuteketezwana mafuta ya wanyama wenu wanono.Sipendezwi na damu ya fahali,wala ya wanakondoo, wala ya beberu.

12. Mnapokuja mbele yangu kuniabudunani aliyewataka mkanyagekanyage nyua zangu?

13. Msiniletee tena matoleo yenu yasiyo na maana;ubani ni chukizo kwangu.Acheni kufanya sikukuu za mwezi mpya,Sabato na mikutano mikubwa ya ibada;sikubali ibada zilizochanganyika na dhambi.

14. Sikukuu zenu za mwezi mpya na nyinginezomoyo wangu wazichukia.Zimekuwa mzigo mzito kwangu,nami nimechoka kuzivumilia.

15. “Mnapoinua mikono yenu kuombanitauficha uso wangu nisiwaone.Hata mkiomba kwa wingi sitawasikia,maana mikono yenu imejaa damu.

Kusoma sura kamili Isaya 1