Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 1:18-31 Biblia Habari Njema (BHN)

18. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Njoni, basi, tuhojiane.Ingawa mna madoa mekundu ya dhambi,mtatakaswa na kuwa weupe kama theluji;madoa yenu yajapokuwa mekundu kama damu,mtakuwa weupe kama sufu.

19. Mkiwa tayari kunitii,mtakula mazao mema ya nchi.

20. Lakini mkikaidi na kuniasi,mtaangamizwa kwa upanga.Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”

21. Jinsi gani mji uliokuwa mwaminifusasa umegeuka kuwa kahaba!Wakati mmoja haki ilitawala humo,lakini sasa umejaa wauaji.

22. Fedha yenu imekuwa takataka;divai yenu imechanganyika na maji.

23. Viongozi wako ni waasi;wanashirikiana na wezi.Kila mmoja anapenda hongo,na kukimbilia zawadi.Hawawatetei yatima,haki za wajane si kitu kwao.

24. Kwa hiyo asema Bwana Mwenyezi-Mungu,Mwenye Nguvu wa Israeli:“Nitawamwagia maadui zangu hasira yangu,nitawalipiza kisasi wapinzani wangu.

25. Nitanyosha mkono wangu dhidi yenu;nitayeyusha uchafu wenu kabisa,na kuondoa takataka yenu yote.

26. Nitawapeni waamuzi wenu kama kwanzana washauri wenu kama pale awali.Ndipo Yerusalemu utakapoitwa ‘Mji wa Uadilifu’utaitwa ‘Mji Mwaminifu’”

27. Mji Siyoni utakombolewa kwa haki,uadilifu utawaokoa watakaotubu humo.

28. Lakini waasi na wenye dhambiwote wataangamizwa pamoja;wanaomwacha Mwenyezi-Mungu watateketezwa.

29. Mtaionea aibu hiyo mialoni mliyoipenda sana;mtafadhaika kwa sababu ya bustani mlizofurahia.

30. Mtakuwa kama mwaloni unaonyauka majani;kama shamba lisilo na maji.

31. Wenye nguvu watakuwa kama majani makavu,matendo yao yatakuwa kama cheche za moto.Watateketea pamoja na matendo yao,wala hapatakuwa na mtu wa kuwaokoa.

Kusoma sura kamili Isaya 1