Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 1:15-25 Biblia Habari Njema (BHN)

15. “Mnapoinua mikono yenu kuombanitauficha uso wangu nisiwaone.Hata mkiomba kwa wingi sitawasikia,maana mikono yenu imejaa damu.

16. Jiosheni, jitakaseni;ondoeni uovu wa matendo yenu mbele yangu.Acheni kutenda maovu,

17. jifunzeni kutenda mema.Tendeni haki,ondoeni udhalimu,walindeni yatima,teteeni haki za wajane.”

18. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Njoni, basi, tuhojiane.Ingawa mna madoa mekundu ya dhambi,mtatakaswa na kuwa weupe kama theluji;madoa yenu yajapokuwa mekundu kama damu,mtakuwa weupe kama sufu.

19. Mkiwa tayari kunitii,mtakula mazao mema ya nchi.

20. Lakini mkikaidi na kuniasi,mtaangamizwa kwa upanga.Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”

21. Jinsi gani mji uliokuwa mwaminifusasa umegeuka kuwa kahaba!Wakati mmoja haki ilitawala humo,lakini sasa umejaa wauaji.

22. Fedha yenu imekuwa takataka;divai yenu imechanganyika na maji.

23. Viongozi wako ni waasi;wanashirikiana na wezi.Kila mmoja anapenda hongo,na kukimbilia zawadi.Hawawatetei yatima,haki za wajane si kitu kwao.

24. Kwa hiyo asema Bwana Mwenyezi-Mungu,Mwenye Nguvu wa Israeli:“Nitawamwagia maadui zangu hasira yangu,nitawalipiza kisasi wapinzani wangu.

25. Nitanyosha mkono wangu dhidi yenu;nitayeyusha uchafu wenu kabisa,na kuondoa takataka yenu yote.

Kusoma sura kamili Isaya 1