Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 1:13-27 Biblia Habari Njema (BHN)

13. Msiniletee tena matoleo yenu yasiyo na maana;ubani ni chukizo kwangu.Acheni kufanya sikukuu za mwezi mpya,Sabato na mikutano mikubwa ya ibada;sikubali ibada zilizochanganyika na dhambi.

14. Sikukuu zenu za mwezi mpya na nyinginezomoyo wangu wazichukia.Zimekuwa mzigo mzito kwangu,nami nimechoka kuzivumilia.

15. “Mnapoinua mikono yenu kuombanitauficha uso wangu nisiwaone.Hata mkiomba kwa wingi sitawasikia,maana mikono yenu imejaa damu.

16. Jiosheni, jitakaseni;ondoeni uovu wa matendo yenu mbele yangu.Acheni kutenda maovu,

17. jifunzeni kutenda mema.Tendeni haki,ondoeni udhalimu,walindeni yatima,teteeni haki za wajane.”

18. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Njoni, basi, tuhojiane.Ingawa mna madoa mekundu ya dhambi,mtatakaswa na kuwa weupe kama theluji;madoa yenu yajapokuwa mekundu kama damu,mtakuwa weupe kama sufu.

19. Mkiwa tayari kunitii,mtakula mazao mema ya nchi.

20. Lakini mkikaidi na kuniasi,mtaangamizwa kwa upanga.Mimi, Mwenyezi-Mungu, nimesema.”

21. Jinsi gani mji uliokuwa mwaminifusasa umegeuka kuwa kahaba!Wakati mmoja haki ilitawala humo,lakini sasa umejaa wauaji.

22. Fedha yenu imekuwa takataka;divai yenu imechanganyika na maji.

23. Viongozi wako ni waasi;wanashirikiana na wezi.Kila mmoja anapenda hongo,na kukimbilia zawadi.Hawawatetei yatima,haki za wajane si kitu kwao.

24. Kwa hiyo asema Bwana Mwenyezi-Mungu,Mwenye Nguvu wa Israeli:“Nitawamwagia maadui zangu hasira yangu,nitawalipiza kisasi wapinzani wangu.

25. Nitanyosha mkono wangu dhidi yenu;nitayeyusha uchafu wenu kabisa,na kuondoa takataka yenu yote.

26. Nitawapeni waamuzi wenu kama kwanzana washauri wenu kama pale awali.Ndipo Yerusalemu utakapoitwa ‘Mji wa Uadilifu’utaitwa ‘Mji Mwaminifu’”

27. Mji Siyoni utakombolewa kwa haki,uadilifu utawaokoa watakaotubu humo.

Kusoma sura kamili Isaya 1