Agano la Kale

Agano Jipya

Isaya 1:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Maono aliyoyaona Isaya, mwana wa Amozi, kuhusu Yuda na mji wa Yerusalemu, nyakati za utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda.

2. Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Sikilizeni enyi mbingu,tega sikio ee dunia.Mimi nimewalea wanangu wakakua,lakini sasa wameniasi!

3. Ngombe humfahamu mwenyewe,punda hujua kibanda cha bwana wake;lakini Waisraeli hawajui,watu wangu, hawaelewi!”

4. Ole wako wewe taifa lenye dhambi,watu waliolemewa na uovu,wazawa wa wenye kutenda maovu,watu waishio kwa udanganyifu!Nyinyi mmemwacha Mwenyezi-Mungu,mmemdharau Mtakatifu wa Israeli,mmefarakana naye na kurudi nyuma.

Kusoma sura kamili Isaya 1