Agano la Kale

Agano Jipya

Hosea 4:5-17 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Wewe utajikwaa mchana,naye nabii atajikwaa pamoja nawe usiku.Nitamwangamiza mama yako Israeli.

6. Watu wangu wameangamia kwa kutonijua,maana wewe kuhani umekataa mafundisho.Nimekukataa kuwa kuhani wangu.Kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako,nami pia nitawasahau watoto wako.

7. “Kadiri makuhani walivyoongezeka,ndivyo wote walivyozidi kuniasi.Basi, nitaigeuza fahari yao kuwa aibu.

8. Wanajishibisha kwa sadaka za watu wangu wenye dhambi.Wana hamu sana ya kuwaona wametenda dhambi.

9. Lakini yatakayowapata watu yatawapata makuhani;nitawaadhibu kwa sababu ya mwenendo wao,nitawalipiza matendo yao wenyewe.

10. Watakula, lakini hawatashiba;watazini, lakini hawatapata watoto,kwa sababu wameniacha mimi Mwenyezi-Mungu,na kufuata miungu mingine.

11. “Divai mpya na ya zamanihuondoa maarifa.

12. Watu wangu huomba shauri kutoka kwa mti;kijiti chao cha ramli ndicho kinachowapa kauli.Nia ya kufanya uzinzi imewapotosha;wamefanya uzinzi kwa kufuata miungu mingine,wakaniacha mimi Mungu wao.

13. Wanatambikia kwenye vilele vya milima;naam, wanatoa tambiko vilimani,chini ya mialoni, migude na mikwaju,maana kivuli chao ni kizuri.“Kwa hiyo binti zenu hufanya uzinzi,na bibiarusi wenu hufanya uasherati.

14. Lakini sitawaadhibu binti zenu wanapofanya uzinzi,wala bibi arusi wenu wanapofanya uasherati,maana, wanaume wenyewe ndio wanaofuatana na wazinzi,na kutambikia pamoja nao katika ibada za uzinzi.Watu hawa watovu wa akili hakika wataangamia!

15. “Ama kweli nyinyi Waisraeli ni wazinzi!Lakini, msiwafanye watu wa Yuda wawe na hatia!Msiende mahali patakatifu huko Gilgali,wala msiende kule Beth-aveni.Wala msiape mkisema,‘Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo!’”

16. Waisraeli ni wakaidi kama punda.Kwa nini basi Mungu ashughulike kuwachunga,kama kondoo kwenye malisho mapana?

17. “Watu wa Efraimu wamejifunga na sanamu.Haya! Waache waendelee tu!

Kusoma sura kamili Hosea 4