Agano la Kale

Agano Jipya

Hosea 2:6-17 Biblia Habari Njema (BHN)

6. Basi, nitaiziba njia yake kwa miiba,nitamzungushia ukuta,asipate njia ya kutokea nje.

7. Atawafuata wapenzi wake,lakini hatawapata;naam, atawatafuta,lakini hatawaona.Hapo ndipo atakaposema,“Nitarudi kwa mume wangu wa kwanza;maana hapo kwanza nilikuwa nafuu kuliko sasa.”

8. Hakujua kwamba ni miminiliyempa nafaka, divai na mafuta,niliyemjalia fedha na dhahabu kwa wingi,ambazo alimpelekea Baali.

9. Kwa hiyo wakati wa mavuno nitaichukua nafaka yangu,nitaiondoa divai yangu wakati wake.Nitamnyang'anya nguo zangu za sufu na kitani,ambazo zilitumika kuufunika uchi wake.

10. Nitamvua abaki uchi mbele ya wapenzi wake,wala hakuna mtu atakayeweza kunizuia.

11. Nitazikomesha starehe zake zote,sikukuu zake za mwezi mwandamo na za Sabato,na sikukuu zote zilizoamriwa.

12. Nitaiharibu mizabibu yake na mitini,anayosema ni malipo kutoka kwa wapenzi wake.Nitaifanya iwe misitu,nao wanyama wa porini wataila.

13. Nitamlipiza sikukuu za Baali alizoadhimisha,muda alioutumia kuwafukizia ubani,akajipamba kwa pete zake na johari,na kuwaendea wapenzi wake,akanisahau mimi.Mimi Mwenyezi-Mungu nasema.

14. Kwa hiyo, nitamshawishi,nitampeleka jangwanina kusema naye kwa upole.

15. Huko nitamrudishia mashamba yake ya mizabibu,bonde la Akori nitalifanya lango la tumaini.Atanifuata kwa hiari kama alipokuwa kijana,kama wakati alipotoka katika nchi ya Misri.

16. “Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Siku hiyo, wewe utaniita ‘Mume wangu,’ na sio tena ‘Baali wangu.’

17. Maana, nitalifanya jina la Baali lisitamkike tena kinywani mwako.

Kusoma sura kamili Hosea 2