Agano la Kale

Agano Jipya

Hosea 2:14-21 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Kwa hiyo, nitamshawishi,nitampeleka jangwanina kusema naye kwa upole.

15. Huko nitamrudishia mashamba yake ya mizabibu,bonde la Akori nitalifanya lango la tumaini.Atanifuata kwa hiari kama alipokuwa kijana,kama wakati alipotoka katika nchi ya Misri.

16. “Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Siku hiyo, wewe utaniita ‘Mume wangu,’ na sio tena ‘Baali wangu.’

17. Maana, nitalifanya jina la Baali lisitamkike tena kinywani mwako.

18. Nitafanya agano na wanyama wa porini, ndege wa angani pamoja na vyote vitambaavyo, wasikuumize. Nitatokomeza upinde, upanga na silaha za vita katika nchi, na kukufanya uishi kwa usalama.

19. Nitakufanya mke wangu milele; uwe wangu kwa uaminifu na haki, kwa fadhili na huruma.

20. Naam, nitakuposa kwa uaminifu, nawe utanijua mimi Mwenyezi-Mungu.

21. “Siku hiyo, mimi Mwenyezi-Mungu nasema,nitaikubali haja ya mbingu ya kunyesha mvua,mbingu nazo zitaikubali haja ya ardhi.

Kusoma sura kamili Hosea 2