Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 7:67-76 Biblia Habari Njema (BHN)

67. Sadaka yake ilikuwa: Sahani moja ya fedha ya kilo moja u nusu na bakuli moja la fedha la gramu 800, kadiri ya vipimo vya hema takatifu; sahani na bakuli vilikuwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka;

68. kisahani kimoja cha dhahabu cha gramu 110 kilichokuwa kimejazwa ubani;

69. fahali mmoja wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

70. beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi;

71. fahali wawili, kondoo madume watano, beberu watano na wanakondoo madume watano wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya amani. Hiyo ndiyo iliyokuwa sadaka ya Ahiezeri mwana wa Amishadai.

72. Siku ya kumi na moja ikawa zamu ya Pagieli mwana wa Okrani, kiongozi wa kabila la Asheri.

73. Sadaka yake ilikuwa: Sahani ya fedha ya kilo moja u nusu na bakuli moja la fedha la gramu 800 kadiri ya vipimo vya hema takatifu vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya nafaka;

74. kisahani kimoja cha dhahabu cha gramu 110 kilichokuwa kimejazwa ubani;

75. fahali mmoja mchanga, kondoo dume mmoja wa mwaka mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;

76. beberu mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuondoa dhambi;

Kusoma sura kamili Hesabu 7