Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 33:47-56 Biblia Habari Njema (BHN)

47. Kutoka Almon-diblathaimu, walisafiri na kupiga kambi yao katika milima ya Abarimu, karibu na Mlima Nebo.

48. Kutoka milima ya Abarimu, walisafiri na kupiga kambi yao katika tambarare za Moabu ngambo ya mto Yordani karibu na Yeriko.

49. Walipiga kambi hiyo karibu na mto Yordani kati ya Beth-yeshimothi na bonde la Abel-shitimu kwenye tambarare za Moabu.

50. Katika tambarare za Moabu, ngambo ya mto Yordani karibu na Yeriko, Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose,

51. “Waambie Waisraeli kwamba mtakapovuka mto Yordani na kuingia katika nchi ya Kanaani,

52. wafukuzeni wenyeji wote wa nchi hiyo mbele yenu. Mtaziharibu sanamu zao zote za mawe na za kusubu na kupabomoa kila mahali pao pa juu pa ibada.

53. Mtaichukua nchi hiyo na kukaa humo kwa sababu nimewapeni muimiliki.

54. Mtaigawanya nchi hiyo kwa kura kufuata familia zenu; eneo kubwa kwa kabila kubwa na eneo dogo kwa kabila dogo.

55. Lakini kama msipowafukuza wenyeji wa nchi hiyo kwanza, basi wale mtakaowaacha watakuwa kama vibanzi machoni mwenu au miiba kila upande, na watawasumbua.

56. Nami nitawafanyeni nyinyi kama nilivyokusudia kuwafanya wao.”

Kusoma sura kamili Hesabu 33