Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 33:34-49 Biblia Habari Njema (BHN)

34. Kutoka Yot-batha, walipiga kambi yao Abrona.

35. Kutoka Abrona, walipiga kambi yao Esion-geberi.

36. Waliondoka Esion-geberi, wakasafiri na kupiga kambi yao katika jangwa la Sini, (yaani Kadeshi).

37. Kutoka Kadeshi, walipiga kambi yao mlimani Hori, mpakani mwa nchi ya Edomu.

38. Kwa agizo la Mwenyezi-Mungu kuhani Aroni alipanda juu ya Mlima Hori, na huko, akafariki mnamo siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arubaini tangu Waisraeli walipotoka nchini Misri.

39. Aroni alikuwa na umri wa miaka 123 alipofariki juu ya Mlima Hori.

40. Mfalme wa Aradi, Mkanaani, aliyekaa Negebu katika nchi ya Kanaani, alipata habari kwamba Waisraeli walikuwa wanakuja.

41. Kutoka Mlima Hori, Waisraeli walipiga kambi yao Salmona.

42. Kutoka Salmona, walipiga kambi yao Punoni.

43. Kutoka Punoni, walipiga kambi yao Obothi.

44. Kutoka Obothi, walipiga kambi yao Iye-abarimu, katika eneo la Moabu.

45. Kutoka Iye-abarimu, walipiga kambi yao Dibon-gadi.

46. Kutoka Dibon-gadi, walisafiri na kupiga kambi yao Almon-diblathaimu.

47. Kutoka Almon-diblathaimu, walisafiri na kupiga kambi yao katika milima ya Abarimu, karibu na Mlima Nebo.

48. Kutoka milima ya Abarimu, walisafiri na kupiga kambi yao katika tambarare za Moabu ngambo ya mto Yordani karibu na Yeriko.

49. Walipiga kambi hiyo karibu na mto Yordani kati ya Beth-yeshimothi na bonde la Abel-shitimu kwenye tambarare za Moabu.

Kusoma sura kamili Hesabu 33