Agano la Kale

Agano Jipya

Hesabu 33:3-12 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Waisraeli waliondoka mjini Ramesesi mnamo siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku moja baada ya Pasaka ya kwanza. Waliondoka kwa uhodari mkubwa mbele ya Wamisri wote,

4. ambao walikuwa wanawazika wazaliwa wao wa kwanza wa kiume aliowaua Mwenyezi-Mungu; kwani Mwenyezi-Mungu alikuwa ameiadhibu hata miungu yao.

5. Basi, Waisraeli waliondoka Ramesesi, wakapiga kambi yao huko Sukothi.

6. Kutoka Sukothi, walipiga kambi yao huko Ethamu, ukingoni mwa jangwa.

7. Kutoka Ethamu, waligeuka na kurudi hadi Pi-hahirothi, mashariki ya Baal-sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli.

8. Waliondoka Pi-hahirothi, wakapita bahari ya Shamu mpaka jangwa la Ethamu; walisafiri jangwani mwendo wa siku tatu, wakapiga kambi yao Mara.

9. Kutoka Mara, walisafiri hadi Elimu; huko Elimu kulikuwa na chemchemi kumi na mbili za maji na mitende sabini, wakapiga kambi yao mahali hapo.

10. Walisafiri kutoka Elimu, wakapiga kambi yao karibu na bahari ya Shamu.

11. Kutoka Bahari ya Shamu walipiga kambi yao katika jangwa la Sini.

12. Kutoka jangwa la Sini, walipiga kambi yao Dofka.

Kusoma sura kamili Hesabu 33